Nenda kwa yaliyomo

Lango:Cote d'Ivoire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu!!!
Welcome

Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

Lango la Cote d'Ivoire
Location on the world map
Location on the world map
Cote d'Ivoire (tamka: kot divwar; kifar.: "Pwani la pembe za ndovu") (Kisw. pia: Kodivaa, Ivory Coast), kwa Kiingereza Ivory Coast ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana kwenye mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini.

Iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha zimeharibika kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Jamii
Wasifu Uliochaguliwa

Alpha Blondy (jina la kulizaliwa: Seydou Koné; * Dimbokoro, Côte d'Ivoire, 1 Januari 1953), ni mwanamuziki wa Reggae na msanii anayerekodi nyimbo zake nyingi kimataifa. Alpha Blondy mara nyingi huimba kwa lugha ya Kidioula ambayo ndio lugha yake ya taifa huku akichanganya Kifaransa na Kiingereza, lakini pia wakati mwingine huimba kwa Kiarabu au Kiyahudi. Mashairi yake yanamaanisha siasa kali yenye mwelekeo na uchangamfu.

Alpha ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tisa, Jina la kuzaliwa ni Seydou Kone amezaliwa mjini Dimbokro mnamo 1953. Alilelewa na bibi yake mzaa mama. Mnamo mwaka 1962, Alpha Blondy alikwenda kukaa na baba yake aliyekuwa anaishi mjini Odienne, Ambapo alikaa kwa muda wa miaka kumi, Baadae akijiunga na shule ya Sainte Elisabeth high school, na kujishughulisha na makundi ya wanafunzi ya Ivory Coast. Hapo ndipo alipo unda bendi. Ingawaje, Upenzi huu uliathiri masomo yake na baadae Blondy alikufukuzwa shule kutokana na maudhulio mabovu shuleni.


Mradi
Makala iliyochaguliwa
Sherehe ya amani katika Bouaké

Serikali ya Côte d'Ivoire (Ivory Coast) inachukua nafasi katika mfumo wa uwakilishi wa uraisi katika jamhuri ya kidemokrasia, ambapo Rais wa Cote d'Ivoire ni mkuu wa nchi na vilevile ni kiongozi wa serikali, na inafuata mfumo wa vyama vingi. Nguvu ya kiutendaji hutimizwa na serikali tu. Suala la utunzi wa sheria hutekelezwa kwa njia ya serikali yenyewe au bunge.

Mji mkuu rasmi tangu 1983 ni Yamoussoukro; hata hivyo, Abidjan unabaki kuwa kitovu cha utawala. Nchi nyingi huweka balozi zao mjini Abidjan, ijapokuwa baadhi yao (ikiwa ni pamoja na Uingereza) wamefunga harakati zao kwa sababu ya fujo zinaoendelea na ushambuliaji dhidi ya Wazungu. Wakazi wanaendelea kupata shida kwa kufuatia vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea.


Picha Iliyochaguliwa

Wanafunzi wa mafunzo ya michezo nchini Abidjan.


Je, wajua...?
  • ... kwamba Cote d'Ivoire iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha kwa jumla vimeharibika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe (2002-2011)?
  • ... kwamba lugha zinazotumika kwa kawaida nchini Cote d'Ivoire ni 65, lakini lugha rasmi ni Kifaransa?
  • ... kwamba Katika Cote d'Ivoire, Uislamu una 38.6%, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki) 32.8%, na dini asilia za Kiafrika 28%?