Huduma zote za Google, zinakufanyia kazi
Ingia katika Akaunti yako ya Google ili ufurahie zaidi huduma zote za Google unazotumia. Akaunti yako hukusaidia ufanye mambo mengi kwa kuweka mapendeleo kwenye hali ya utumiaji katika Google na kukupa uwezo wa kufikia taarifa zako muhimu kwa njia rahisi mahali popote.
Inakusaidia
Unapoingia katika akaunti, huduma zote za Google unazotumia hufanya kazi kwa pamoja ili kukusaidia kutekeleza majukumu ya kila siku kama vile kusawazisha akaunti yako ya Gmail na programu za Kalenda na Ramani ya Google ili kuhakikisha kila wakati unafuata ratiba vyema.
Zimebuniwa kwa ajili yako
Bila kuzingatia kifaa au huduma ya Google unayotumia, akaunti yako hukupa hali nzuri ya utumiaji ambayo unaweza kudhibiti na kuwekea mapendeleo wakati wowote.
Inakulinda
Akaunti yako ya Google inalindwa kwa vipengele bora vya usalama ambavyo husaidia kutambua na kuzuia hatari kiotomatiki kabla hazijakufikia.
Tayari kukusaidia
Akaunti yako ya Google hukusaidia uokoe muda kwa kuweka kiotomatiki manenosiri, anwani na maelezo ya malipo kwa kutumia taarifa ulizohifadhi kwenye akaunti yako.
Unapoingia katika Akaunti yako ya Google, Huduma zote za Google unazotumia hufanya kazi pamoja ili kukusaidia ufanye mambo zaidi. Kwa mfano, safari za ndege unazothibitisha kwenye kikasha cha Gmail yako zitasawazishwa kiotomatiki na programu ya Kalenda na Ramani ya Google ili kukusaidia ufike kwenye uwanja wa ndege kwa wakati.
Iwe ni kuendelea kutazama video za YouTube kwenye vifaa mbalimbali au kupata kwa urahisi anwani pamoja na programu unazopenda kwenye Duka la Google Play, mchakato wa kuingia katika akaunti mara moja unakuruhusu upate hali rahisi ya utumiaji kwenye huduma mbalimbali za Google. Akaunti yako ya Google pia hufanya iwe rahisi kwako kuingia katika programu za wengine kwa njia salama na haraka, kwa hivyo mapendeleo yako yanapatikana hata nje ya Google.
Kwa ajili yako
Unaweza kufikia data na mipangilio yako kwa kugusa mara moja tu. Gusa tu picha yako ya wasifu na ufuate kiungo ili “Udhibiti Akaunti yako ya Google”. Ukiwa kwenye picha yako ya wasifu, unaweza pia kuwasha Hali Fiche, kuingia au kuondoka kwenye akaunti kwa urahisi.
Tunajua kuwa suala la faragha halishughulikiwi kwa njia moja pekee. Kwa hivyo, kila Akaunti ya Google huwa na vidhibiti na zana rahisi kutumia kama vile Ukaguzi wa Faragha ili uweze kuchagua mipangilio ya faragha inayokufaa. Unaweza pia kudhibiti data inayohifadhiwa kwenye akaunti yako kwa kutumia vidhibiti vya kuwasha au kuzima vilivyo rahisi kutumia, na hata ufute data yako kulingana na tarehe, bidhaa na mada.
Akaunti yako ya Google hukupa eneo moja kuu na salama la kuhifadhi taarifa zako binafsi — kama vile manenosiri, kadi za mikopo na anwani — kwa hivyo unaweza kuzipata wakati wowote kwenye intaneti unapohitaji.
Kulinda taarifa zako kwa njia salama na ya faragha
Akaunti yako ya Google hulinda kiotomatiki taarifa yako binafsi na huiweka salama na kwa faragha. Kila akaunti huwa na vipengele thabiti kama vile vichujio vya taka ambavyo huzuia asilimia 99.9 ya barua pepe hatari kabla hazijakufikia na arifa za usalama zilizowekewa mapendeleo zinazokuarifu kuhusu shughuli za kutiliwa shaka na tovuti hasidi.
Zana hii rahisi hukupa mapendekezo yanayokufaa ili kusaidia kulinda akaunti yako.
Akaunti yako ya Google huwa na Kidhibiti cha Manenosiri kilichojumuishwa ambacho huhifadhi manenosiri yako katika eneo moja kuu ambako ni wewe tu unaweza kufikia.